Mfungaji bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita Meddie Kagere tayari ametua nchini ambapo leo ataungana na wachezaji wengine kwenye kambi ya muda Sea Scape Hotel jijini Dar es salaam
Kagere amerejea nchini akiwa na deni kubwa la kuhakikisha mafanikio aliyopata msimu uliopita anayaendeleza
Kagere aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu akiwa amefunga mabao 23
Pia ndiye aliyekuwa kinara wa mabao kwenye kikosi Simba katika michuano ya ligi ya mabingwa akiwa ametupia kambani mabao sita
Simba inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam keshokutwa Jumatatu kuelekea Afrika Kusini kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya
ADVERTISE HERE