Mshambuliaji Adam Salamba yuko Afrika Kusini kujiunga na klabu ya TS Sporting FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza
Salamba bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Simba hivyo msimu wake wa kwanza ataichezea timu hiyo kwa mkopo
Mshambuliaji huyo aliyetua Simba msimu uliopita akitokea klabu ya Lipuli Fc, alishindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania Bara ambacho kilisheheni washambuliaji nyota walioongozwa na nahodha John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi
Hii ni nafasi nzuri kwake kuonyesha makali na pengine anaweza kurejeshwa kikosini msimu ujao
Salamba mwenye umri wa miaka 19, amesema ataitumia nafasi hiyo ili kujitengenezea mazingira mazuri zaidi ya kujiunga na timu kubwa
cut"Licha ya kutopata nafasi ya kutosha Simba, lakini niliweza kujifunza mambo mengi ambayo naamini yatanisaidia kufanya vizuri hapa," amesema
"Changamoto zilizozipata nimeshazisahau, sasa najipanga ili niweze kufanya vizuri"
Nafasi ya Salamba kwenye kikosi cha Simba ilizidi kuwa finyu baada ya mabingwa hao wa nchi kusajili washambuliaji wawili Mbrazil Wilker Da Silva na Mcongomani Deo Kanda licha ya kuondoka Emmanuel Okwi