Kikosi cha Simba kitaondoka jijini Dar es salaam wakati wowote kuelekea Afrika Kusini kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya
Wachezaji wa kigeni wa mabingwa hao wa Tanzania Bara wanatarajiwa kuanza kuwasili leo kuungana na wenzao walioko hapa nchini
Ikiwa Afrika Kusini, Simba inatarajiwa kucheza michezo kadhaa ya kirafiki ambapo Mtendaji Mkuu Crescentius Magori amesema tayari wamepokea maombi kutoka timu mbalimbali zinazotaka kujipima na Simba nchini humo
Hata hivyo Magori amesema watakapofika nchini humo ndio watafahamu ni timu gani wacheze nazo
"Tunaenda kuweka kambi Afrika Kusini lakini pia tuna mpango wa kucheza mechi za kirafiki kwa ajili ya kujipima," amesema
"Mpaka sasa sijui tutacheza na timu ipi, sababu kuna timu kadhaa zinataka kucheza mechi na sisi"
"Tutakapofika huko kuanza maandalizi, ndipo tutafanya maamuzi tutacheza na timu ipi"
Simba imekuwa maarufu barani Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita, ikifanikiwa kutinga robo fainali