Beki mpya wa Simba Gadiel Michael amesema amefurahi kujiunga na timu bora nchini Tanzania na atahakikisha anafanya vizuri zaidi ya pale alipoishia Yanga
Gadiel alitambulishwa jana baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili
Kuhusu changamoto ya namba mbele ya nahodha msaidizi, Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr', Gadiel amesema uamuzi wa nani acheze uko mikononi mwa kocha Patrick Aussems
"Nimekuja Simba huku nikifahamu timu hii imekamilika, hivyo napaswa kujituma ili kumshawishi kocha aweze kunipa nafasi," amesema
"Namuomba Mungu nifanye kile ambacho wamekilenga kwangu"
Ujio wa Gadiel umemuondoa beki Mghana Asante Kwasi ambaye huenda akaibukia klabu ya Biashara United inayonolewa na kocha wa zamani wa Lipuli na Mbao Fc, Amri Said
ADVERTISE HERE