Niko tayari kukutana na Mo - Kilomoni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Jul 2019
Niko tayari kukutana na Mo - Kilomoni

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Simba, Hamis Kilomoni ametaka kukutanishwa na mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji (Mo) mezani ili kuweka mambo sawa kwa maslahi ya klabu.

Kilomoni amekuwa akionyesha msimamo wake juu ya mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa Simba amesema yuko tayari kukaa mezani na mwekezaji huyo ili kuweka mambo sawa.

"Sina tatizo na Mo, ndiyo sababu nimesema akitaka tukae mezani nitafanya hivyo, na si MO tu hata akitokea mwekezaji mwingine yoyote Simba nitakaa naye mezani kwa maslahi ya klabu.

"Hivyo kama MO atapenda aje tuzungumze, kikubwa ni mipango ya maendeleo iwe wazi na kila Mwana Simba haifahamu," alisema Kilomoni na kufafanua.

"Mabadiliko Simba ni ya watu siyo ya mtu, hivyo yanahitaji msukumo wa pamoja, japo kwenye wengi pana mengi, wengine waongo, wengine wakweli na wengine watazamaji," alisema Kilomoni.

Alisema kama MO atakuwa tayari kukaa mezani, moja ya mambo watakayozungumza naye ni msimamo wa Serikali ambao unataka klabu ya Simba kuwa na wawekezaji kuanzia watatu kuendelea ambao watagawana asilimia 49 ya hisa

"Klabu haiwezi kuwa na mwekezaji mmoja pekee, katika asilimia 49 ya hisa, muongozo tuliopewa ni kwamba wawekezaji wasiopungua watatu watagawana asilimia 49 ya hisa na 51 zitakazobaki zitakuwa za wanachama na kila mwekezaji atakayehitaji kuwekeza Simba msimamo wa Serikali ndiyo huo," alisema Kilomoni.

Alipoulizwa kwanini yeye asimtafute MO ili wakae mezani kuweka mambo sawa kwa maslahi ya Simba, Kilomoni alisema hawezi kufanya hivyo.

"MO ni mwanangu kiumri pamoja na kwamba anataka kuwekeza Simba hivyo siwezi kumtafuta, ila akitaka tukae pamoja tuijenge Simba basi anitafute niko tayari na ninaamini tutafikia muafaka," alisema.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
9h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
9h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
12h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’