Hii inaweza kuwa habari njema kwa Wanamsimbazi ambao wengi walikuwa hawaridhishwi na uwezo wa mlinzi wa kulia wa timu hiyo Zana Coulibaly
Zana aliyetua nchini wiki iliyopita, amerejea kwao baada ya viongozi wa Simba kuachana na mpango wa kumpa mkataba mpya
Imeelezwa Simba imepanga kusajili beki mwingine wa kigeni mwenye uwezo mkubwa ambaye atasaidiana na Shomari Kapombe
Usajili wa Zana mwezi Disemba 2018 ulipokewa kwa shangwe na mashabiki wa Simba
Hata hivyo alipoteza imani ya mashabiki baada ya kiwango chake kutotabirika
ADVERTISE HERE