Simba imepata bahati ya kuwa na walinda lango hodari ambao kwa nyakati zao wamekuwa tegemeo sio kwa klabu tu bali hata kwa timu ya Taifa
Miongoni mwa walinda lango wanaokumbukwa zaidi ambao walipata mafanikio makubwa kwenye klabu ya Simba na timu ya Taifa ni Mohammed Mwameja na Juma Kaseja
Mwameja alipachikwa jina la 'Tanzania One' kutokana na umahiri wake langoni mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90
Baada ya Mwameja kuondoka miaka michache baadae akaibuka Juma Kaseja ambaye alianza kuitumikia Simba na kuwa mlinda lango namba moja akiwa na miaka 18 tu
Umahiri wake langoni pia ulipelekea akarithishwa jina la 'Tanzania One' ambalo alipewa Mwameja
Sasa klabu ya Simba ina Aishi Manula ambaye hakuna ubishi kuwa ni 'Tanzania One'

Nchini Misri kwenye michuano ya Afcon, Manula alidhihirisha ubora wake kwenye mchezo dhidi ya Senegal ambapo katika mchezo huo aliokoa mipira ya hatari nane iliyokuwa inaelekea langoni
Amekuwa kipa bora wa ligi kuu kwa misimu mitatu mfululizo na bila shaka hana mpinzani
Licha ya ujio wa Beno Kakolanya kwenye kikosi cha Simba, bado hakuna namna mlinda lango huyo ataweza kumuweka nje Manula
Simba imejipambanua kuwa na utamaduni wa kutoa walinda lango bora