Simba yaandaa wimbo maalum wa Simba Day

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Jul 2019
Simba yaandaa wimbo maalum wa Simba Day

Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema klabu hiyo imejipanga kuandika Historia mpya siku ya tamasha la SImba Day litakalofanyika August 08 uwanja wa Taifa

Aidha Magori amesema maandalizi yanaendelea ambapo Msemaji wa klau hiyo Haji Manara amepewa kazi maalum ya kuandaa wimbo wa Simba

Kuhusu kambi Magori amesema Simba itakwenda nje ya nchi, na watatangaza sehemu wanayokwenda baada ya maandalizi kukamilka

"Tutaenda kufanya mazoezi nje ya nchi kujiandaa na msimu ujao wa mashindano"

"Mambo yakiwa tayari tutawaambia ni nchi gani tutaenda kwa ajili ya kambi ya maandalizi," amesema

"Simba Day itakavyokuwa mwaka huu haijapata kutokea, ni funga kazi. Tumempa kazi Manara kuandaa wimbo maalum wa Simba"

"Kabla ya Simba Day, utapigwa kwenye vituo vya Radio na TV na mitandaoni ili siku ya Simba Day kila shabiki aweze kuimba"

"Wimbo huo utakuwa unapigwa kabla ya mechi za Simba ili mashabiki ambao wapo uwanjani wapate moto kuelekea kwenye mechi"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’