Wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki kwenye michuano ya CECAFA Challenge inayopigwa nchini Kenya, Zanzibar Heroes wametinga fainali ya michuano hiyo baada ya kuwaondosha mabingwa watetezi Uganda Cranes kwa mabao 2-1.
Zanzibar Heroes sasa watakutana na Kenya kwenye mchezo wa fainali keshokutwa Jumapili.
Zanzibar walifunga mwanzo kupitia Abdul Azizi Makame dakika ya 25 kisha Derrick Nsibambi akaisawazishia Uganda kabla Mohammed Issa Juma hajapachika wavuni bao la pili la Zanzibar .
Wenyeji Kenya walifuzu baada ya kuwashinda Burundi kwa bao la muda wa ziada lililofungwa na kiungo wa kati Whyvonne Isuza.
Katibu mtendaji wa baraza la taifa la michezo Zanzibar Khamis Ali Mzee amefurahishwa na matokeo hayo huku akifunguka kwamba Zanzibar wanarejea kwa nguvu FIFA kudai uwanachama kamili.
HEKO ZANZIBAR!

ADVERTISE HERE