Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi raia wa Uganda amethibitisha kuwa sio straika wa mchezo mchezo baada ya kuweka rekodi ambayo imezishinda timu 14 za Ligi Kuu wakiwemo watetezi, Yanga.
Okwi amefunga mabao sita katika Ligi ambayo ni mengi zaidi ya timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo.
Mpaka mechi za mzunguuko wa tano zinakamilika, ni timu mbili tu ambazo zimefunga mabao zaidi ya sita Ligi Kuu ambazo ni Prisons ya Mbeya yenye mabao manane na Simba yenyewe ambayo ina 14.
Timu za Mbao FC na Singida United ndiyo pekee ambazo zimeweza kufunga mabao sawa na Okwi ambapo kila moja ina mabao sita.
Yanga yenye mastraika ghali zaidi Ligi Kuu ina mabao manne tu Ligi Kuu, idadi ambayo ni pungufu ya ile ya Okwi ambaye ametua Simba kwa mara ya tatu msimu huu.
Timu nyingine zenye mabao pungufu ya Okwi ni Kagera Sugar (1), Ruvu Shooting (3), Majimaji (3), Mwadui (5), Njombe (3), Lipuli (3), Ndanda (3), Mbeya City (5), Yanga (4), Azam (4).
Wakati Okwi akiweka rekodi hiyo, timu za Singida United na Mbao FC zimeendeleza makali yao Ligi Kuu baada ya kuwa timu pekee ambazo zimefunga angalau bao moja kwenye kila mchezo.
Singida ilivunja rekodi ya Azam ya kutoruhusu bao lolote msimu huu baada ya sare ya bao 1-1 juzi Jumamosi. Kabla ya hapo Singida ilikuwa imepata angalau bao moja kwenye mechi zote nne za mwanzo dhidi ya Mwadui, Mbao, Stand United na Kagera Sugar.
Mbao kwa upande wao licha ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Prisons, imeweka rekodi ya kufunga pia kila mchezo. Awali ilifunga angalau bao moja dhidi ya Kagera Sugar, Singida United, Mtibwa Sugar na Simba.

ADVERTISE HERE