Kahata ni zaidi ya Niyonzima - Matola

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Jul 2019
Kahata ni zaidi ya Niyonzima - Matola

Kocha wa Polisi Tanzania Selemani Matola amesema anaamini usajili wa kiungo Francis Kahata umefanywa wakati muafaka na klabu ya Simba

Kahata alikamilisha usajili wa kutua Simba jana akisaini mkataba wa miaka miwili

Kiungo huyo wa Kimataifa wa Kenya aliyetokea klabu ya Gor Mahia, amesajiliwa kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima ambaye hakuongezwa mkataba

Matola amesema kiufundi Kahata na Niyonzima wanafanana vitu vingi lakini Kahata amemzidi Mnyarwanda huyo katika mambo kadhaa

"Kahata ana nguvu na pia ni mzuri kwenye kukaba, Niyonzima anaifaidisha timu zaidi inapokuwa inashambulia," amesema

"Kama Simba wamemsajili Kahata ili kuchukua nafasi ya Niyonzima watakuwa wamefanya jambo sahihi"

Kahata Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheza eneo la kiungo

Ni miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya kilichoshiriki Afcon

Akiwa Gor Mahia, alishinda Kombe la Ligi Kuu mara tatu, kiungo bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Kenya mara mbili na mchezaji bora wa msimu 2018/2019 wa Gor Mahia

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
39m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’