Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara anaamini msimu ujao ubingwa wa ligi kuu utarudi Msimbazi kwa msimu wa tatu mfululizo kutokana na usajili kabambe uliofanywa na mabingwa hao watetezi
Baada ya jana kumtambulisha kiungo Ibrahim Ajib, leo Simba imemshusha kiungo kutoka Gor Mahia Francis Kahata ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili
"Huu ni usajili kwa ajili ya ligi ya mabingwa barani Afrika," amesema Manara
"Ni usajili kwa ajili ya ya Al Ahly,Mazembe na wakubwa wenzetu, na sio usajili wa kushindana na Yanga"
"Hatuna sababu ya kukosa ubingwa wa ligi kuu na pengine tunaweza kufika hata nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao"
Mpaka sasa Simba imekamilisha usajili wa nyota tisa wa kigeni, nafasi moja ikiwa bado inasubiri kujazwa
Wachezaji wa kigeni waliosajiliwa Simba mpaka sasa ni Tairone Santos da Silva, Wilker Henrique da Silva, Gerson Fraga Viera, Shariff Elden Shiboub, Deo Kanda, Francis Kahata, Paschal Wawa, Clatous Chama na Meddie Kagere