Yanga inaonekana imekata pumzi katika jitihada za kumbakisha beki wao Gadiel Michael ambaye amegoma kusaini mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo
Hii ni nafasi kwa mabingwa wa nchi Simba kumnasa beki huyo ili achukue nafasi ya Asante Kwasi ambaye hataongezwa mkataba
Gadiel anaweza kuongeza kitu kwenye safu ya ulinzi na pia atampunguzia Tshabalala majukumu kwani msimu uliopita nahodha huyo msaidizi alicheza mechi nyingi bila kupumzishwa hali iliyopelekea acheze chini ya kiwango michezo ya mwishoni mwa msimu
Uongozi wa Simba umekanusha kumsajili beki huyo lakini inaelezwa jambo lolote linaweza kutokea ndani ya siku mbili hizi
ADVERTISE HERE