Unapozungumzia wachezaji Mohammed Hussein, Jonas Mkude, Said Ndemla na Ibrahim Ajib ni wachezaji waliopita sehemu nyingi pamoja katika historia ya maisha yao ya soka
Wote walilelewa katika kikosi cha timu ya vijana na Simba na wameendelea kuwa zao la Simba
Ingawa Ajib aliondoka mwaka 2017 kujiunga na Yanga, kurejea kwake ni kama amerudi nyumbani

Tshabalala nahodha msaidizi wa Simba amemkaribisha Ajib kwa kuwambia 'Karibu Tena' kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
Ajib ametambulishwa mapema leo na uongozi wa Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili
ADVERTISE HERE