Mapema wiki hii Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori alisema wiki hii ni mbaya sana kwani inaweza kusababisha baadhi ya watu wakazimia
Hilo limeanza kuthibitishwa leo na uongozi wa Simba baada ya kumtambulisha Ibrahim Ajib aliyekuwa mchezaji tegemeo klabu ya Yanga
Wakati Ajib akitua rasmi Msimbazi, inaelezwa beki Gadiel Michael naye anaweza kufuata njia hiyo baada ya kuwagomea Yanga kuongeza mkataba
Aidha, Simba bado haijatambulisha nyota wawili wa Kimataifa kazi ambayo huenda ikafanywa siku ya kesho Alhamisi na Ijumaa
Miongoni mwa nyota hao ni kiungo Francis Kahata ambaye inaelezwa tayari amemalizana na uongozi wa Simba nchini Misri
ADVERTISE HERE