Baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Kaizer Chiefs kiungo James Kotei amewaaga mashabiki wa Simba akiwaachia ujumbe kuwa waendelee kuisapoti timu kwa nguvu moja
"Wakati najiandaa kuanza changamoto mpya ya maisha ya soka, sitaisahau klabu ya Simba," ameandika Kotei
"Sitausahau mji wa Dar es salaam na muhimu sitaisahau lugha ya kiswahili ambayo nilikuwa nimeanza kuifahamu"
"Nawapenda wote, msiache kuiunga mkono Simba nyakati zote, iwe jua au mvua"
"Naamini siku moja tutakutana tena, nawashukuru kwa kila kitu"
ADVERTISE HERE