Ninje aunga mkono uwekezaji kwenye timu za soka nchini

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Jun 2019
Ninje aunga mkono uwekezaji kwenye timu za soka nchini

Wiki iliyopita Mfanyabiashara Rostam Aziz ambaye ni Mwanachama wa Yanga alitoa maoni ya kuwa haungi mkono timu za soka zenye wanachama wengi kuendeshwa kwa kumilikiwa na mtu mmoja au kufadhiliwa

Rostam aliishauri timu yake ya Yanga kujiepusha na mfumo wa kumilikiwa na mtu mmoja huku akikosoa mfumo unaotumiwa na mabingwa wa Tanzania Bara, Simba

Wadau mbalimbali wamepinga maoni ya Bilionea huyo huku wengi wakimkosoa kuwa hafahamu masuala ya uendeshaji wa soka la kisasa

Miongoni mwa waliotoa maoni ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Ammy Ninje

Ninje amesema Serikali imetambua umuhimu uwekezaji katika mpira wa miguu na ndio maana ikaunda Sheria kusimamia utaratibu huo

Ninje ameeleza kuwa kama serikali tayari imeshaweka utaratibu mzuri wa mgawanyo wa hisa kwa mwekezaji na wanachama hivyo ni vizuri ukafuatwa.

"Tunahitaji kubadilika ila tusikurupuke, tuwape timu wawekezaji ili tuone baada ya muda kama tutapiga hatua, kwa mfano Simba tayari wapo huko na mwekezaji ana asilimia 49, tumpe nafasi ya kufanya mabadiliko ili mwisho wa siku tuone tutafika wapi," amesema

Ammy Ninje ameongeza kuwa hata vilabu vikubwa vilivyofanikiwa barani Ulaya ni vya wanachama lakini vilihama kutoka kwenye mfumo huo na kwenda kwenye uwekezaji na ndio maana vina nguvu uwanjani na kiuchumi kiujumla.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’