Jina la kiungo James Kotei ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuwa hatakuwemo kwenye kikosi cha ti
Jina la kiungo James Kotei ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuwa hatakuwemo kwenye kikosi cha Simba msimu ujao baada ya uongozi kuamua kutomuongeza mkataba
Hata hivyo inaelezwa kocha Patrick Aussems amependekeza mchezaji huyo aongezwe mkataba
Kwa hakika kama kweli Simba itaachana na huyu mwamba mashabiki wataumia sana
Ubora wa safu ya ulinzi ya Simba msimu uliopita ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Kotei nafasi ya kiungo mkabaji kwani aliyafanya vyema majukumu yake ya kuwalinda mabeki wa kati
Ni kiungo ambaye hakupata umaarufu sana Msimbazi lakini kazi aliyoifanya ni kubwa
Simba imemsajili kiungo mkabaji Sharif Eldin Shiboub kutoka Sudan ambaye anatajwa kuchukua nafasi ya mwamba huyu kutoka Ghana
Kotei yuko kwao Ghana kwa ajili ya mapumziko huku akiwa na matumaini ya kupigiwa simu na viongozi wa Simba
"Kwa sasa mimi nipo mapumziko tu huku nyumbani, ninacheza na watoto na familia yangu kiujumla sifahamu lolote juu ya usajili wangu," Kotei amenukuliwa na Championi
"Hadi sasa sijapata simu yoyote ile kutoka kwa kiongozi yeyote wa Simba jambo ambalo linanifanya nisielewe juu ya suala la kurudi kwa msimu ujao, labda tuendelee kusubiri kuona inakuwaje hadi siku za mapumziko zitakapoisha"
Simba inapaswa kukamilisha usajili wa michuano ya CAF kabla ya Julai 01, 2019