Nidhamu yatajwa kumkwamisha Juuko Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Jun 2019
Nidhamu yatajwa kumkwamisha Juuko Simba

Anapokuwa timu ya Taifa ya Uganda, beki Juuko Murshidi ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa timu hiyo

Akiwa na kikosi cha Uganda Cranes nchini Misri, Juuko alin'gara kwenye mchezo dhidi ya DR Congo, mchezo ambao Uganda ilishinda kwa maao 2-0

Lakini katika misimu minne aliyokuwa na Simba, Juuko alikosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza

Wengi wamekuwa wakijiuliza kwa nini Juuko anapokuwa timu ya Taifa anafanya vizuri lakini awapo klabuni haonekani

Sababu kubwa ya Mganda huyo kutoaminiwa na makocha wengi waliopita Simba ni nidhamu yake

Licha ya ubora wake, Juuko anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao sio wafuatiliaji wa yale wanayoelekezwa na walimu

Je anafanya makusudi? kwani hali ni tofauti anapokuwa na timu ya Taifa

Juuko amefungashiwa virago kunako klabu ya Simba baada ya kocha Patrick Aussems kupendekeza aachwe

Sio yeye tu, inaelezwa Aussems alipendekeza nyota waliokuwa na nidhamu mbovu waachwe bila ya kujali majina yao

Simba imesajili mabeki wawili Gerson Vieira na Kennedy Juma na hivyo kuondoa uwezekano wa Mganda huyo kufikiriwa kurejea Msimbazi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
19h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’