Miraji hahofii ushindani wa namba Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Jun 2019
Miraji hahofii ushindani wa namba Simba

Simba ina kikosi kilichojaa nyota wengi hali iliyopelekea baadhi ya wachezaji kushindwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza licha ya kuwa na ubora

Hapa unazungumzia wachezaji kama Adam Salamba, Said Ndemla, Mohammed Ibrahim 'Mo', Rashidi Juma na wengine ambao wamekuwa na nafasi finyu kwenye kikosi cha kwanza

Hivi karibuni Simba ilisajili nyota mwingine mzawa Miraji Athumani ambaye ataungana na wachezaji wengine wazawa waliosajiliwa kama Ibrahim Ajib, Kennedy Juma na Beno Kakolanya

Miraji aliyeanzia soka lake kwenye kikosi cha timu ya vijana ya Simba, amerejea akitokea klabu ya Lipuli Fc

Winga huyo aliyekuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kabla ya kuachwa kwenye mchujo wa pili, ametua Simba baada ya usajili wake kupendekezwa na kocha Patrick Aussems

Miraji anatajwa kuchukua nafasi ya Shiza Kichuya aliyeuzwa nchini Misri

Miraji amesema anafahamu haitakuwa kazi rahisi kupenya kwenye kikosi cha kwanza cha Simba kutokana na ubora wa wachezaji wa timu hiyo lakini anaamini kama atajituma na kufuata maelekezo atakayopewa na benchi la ufundi atakuwa na nafasi

"Siwezi kukata tamaa imani yangu nakwenda kukutana na changamoto ambayo natakiwa kuikabili na kushinda ili niweze kutimiza malengo yangu ya kucheza," amesema

"Nafahamu wachezaji ambao wapo Simba ni wakubwa na wana uzoefu lakini nitakuwa namsikiliza kocha anataka nifanye nini katika na kufanya kazi"

"Narejea Simba kwa mara ya pili, mara ya kwanza nilionekana mdogo nilipandishwa kutoka timu ya vijana kwa maana hiyo ni mzoefu na nafahamu mambo mengi na hata ukubwa na presha ya timu naifahamu"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’