Msemaji wa Simba Haji Manara amesisitiza kuwa timu hiyo inasajili kwa kuangalia zaidi anga za kimataifa na sio ligi ya ndani
Manara ametoa kauli hiyo baada ya Simba kumtambulisha beki kutoka Brazil Gerson Fraga Vieira aliyesaini mktaba wa miaka miwili
Manara amesema hawana wasiwasi na wapinzani wao Yanga kwani wamekuwa wakiwafunga kila siku, lakini wanaimarisha timu ili iweze kuchuana na vigogo wengine wa soka barani Afrika
"Kama Yanga tunawafunga kila siku, kama Mabingwa sisi ndio wenye kombe, na huku Afrika Mashariki na ya kati sisi ndio Baba lao,tukiwa mabingwa wa kihistoria wa ukanda wote huu," amesema
"Sasa tunasajili kuangalia viwango vya Al Alhly, Mamelodi, Esperance, Mazembe na miamba mingine ya Afrika"
"Lengo letu kwa sasa ni ubingwa wa Afrika"