Simba yatumia kampuni maalum 'kusaili' wachezaji wa kigeni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Jun 2019
Simba yatumia kampuni maalum 'kusaili' wachezaji wa kigeni

Mashabiki wa Simba wamekuwa na shauku kubwa ya kufahamu wachezaji wapya wa kigeni waliosajiliwa na timu hiyo hasa baada ya kuibuka taarifa kuwa mabingwa hao wa Tanzania Bara wamekusudia kuacha nyota saba wa kigeni

Mpaka sasa ni nyota wawili tu wa kigeni kiungo Sharaf Eldin Shiboub na mshambuliaji raia wa Brazil Wilker Henrique da Silva waliosaini

Uongozi wa Simba uko makini na mchakato wa usajili wa nyota hao wa kigeni ambapo inaelezwa unatumia kampuni maalum kuwafuatilia

Wengi wamejiuliza Simba imeweza vipi kujiridhisha na uwezo wa mfano Wilker ambaye alikuwa akicheza Brazil timu ya madaraja ya chini

Kazi kubwa imefanywa na kampuni hiyo ambayo ilipewa kazi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji 'Mo'

Inaelezwa Simba ina nyota wengine wawili kutoka Brazil ambao huenda wakapewa mikataba

Jambo jema ni kwamba usajili wa Simba unazingatia zaidi ushiriki wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao, hivyo nyota wapya hasa wa kigeni kigezo namba moja ni kujiridhisha na uwezo wao

Mwenyekiti wa Simba Swedi Mkwabi amesema mchakato wa usajili uko ukingoni na pengine mwishoni mwa wiki nyota wote watakaoitumikia Simba msimu ujao watakuwa wanafahamika

Leo Simba itaendelea na utambulisho wa wachezaji waliosaini mikataba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’