Chama afurahia maboresho kikosi cha Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Jun 2019
Chama afurahia maboresho kikosi cha Simba

Kiungo Clatous Chota Chama 'CCC' maarufu kama Mwamba wa Lusaka yuko kwao nchini Zambia akiendelea na mapumziko baada ya kumaliza msimu wake wa kwanza Simba kwa mafanikio makubwa

Licha ya kutokuwepo nchini, Chama amefichua kuwa anafuatilia kila kinachoendelea Msimbazi na amefurahishwa na maboresho ya kikosi cha Simba yanaofanywa na uongozi

Chama amesema malengo ya msimu ujao ni kupata mafanikio zaidi na anaamini hilo litawezekana kutokana na usajili unaofanywa na viongozi wa Simba

"Ninayo furaha kuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu uliopita na natarajia hata msimu ujao nitakuwapo lakini kinachovutia ni namna kikosi kinavyoboreshwa," Chama amenukuliwa na Mwanaspoti

"Kwa sasa nipo mapumzikoni, lakini nafuatilia kila kitu na ninaamini maboresho yanayofanyika Simba yataifanya iwe tishio zaidi kuliko msimu uliopita na huenda tukatetea tena taji na kutikisa Afrika"

Aidha Chama amesema hahofii mbwembwe za usajili zinazofanywa na watani zao Yanga kwani anaamini kikosi cha Simba ni imara zaidi na kitaendelea kuwa bora dhidi ya wapinzani wao

Hadi sasa Simba imekamilisha usajili wa nyota wanne wapya wakiwamo wawili wa kigeni ambao ni straika Wilker Henrique Da Silva kutoka Brazili na Msudan Shiboub Sharaf Eldin ambaye ni kiungo mshambuliaji.

Wengine ni kipa Beno Kakolanya na mshambuliaji Miraj Athuman walikuwa Yanga na Lipuli, huku nyota wao wa zamani aliyekuwa Yanga, Ibrahim Ajibu akitajwa naye keshasaini mkataba wa miaka miwili.

Zoezi la usajili huenda likakamilishwa mwishoni mwa wiki hii

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’