Amunike alaumiwa kumuweka Nyoni nje

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Jun 2019
Amunike alaumiwa kumuweka Nyoni nje

Kutopangwa kwa kiraka Erasto Nyoni dhidi ya Senegal jana kunatajwa kuwa sababu ya Stars kupoteana sehemu ya katikati na kujikuta ikishambuliwa kwa muda wote wa mchezo wa kwanza wa kundi C michuano ya Afcon ambao Stars ilikubali kipigo cha mabao 2-0

Pamoja na ubora wa Senegal, wadau na wachambuzi mbalimbali wa soka nchini wanaamini Nyoni alipaswa kucheza mchezo wa jana

Kocha Emmanuel Amunike alimtumia David Mwantika sehemu ya ulinzi

Mwantika aliongezwa kikosi cha Stars kuchukua nafasi ya Aggrey Moris aliyeumia siku chache kabla ya michuano ya Afcon kuanza

Upande wa viungo wa kati Amunike aliwatumia Feisal Salum 'Fei Toto' na Mudathir Yahya

Fei Toto hakuwa na mchezo mzuri na alilazimika kumtoa kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika

Wengi wanaamini Nyoni alipaswa kucheza nafasi ya kiungo au beki wa kati ashirikiane na Yondani

"Tunaheshimu uwezo wa Senegal, ni timu namba moja kwa ubora barani Afrika, pia tunaheshimu uamuzi wa kocha Amunike kuanza na kikosi kilichocheza lakini tunadhani uzoefu wa mchezaji kama Erasto Nyoni ulihitajika pale katikati," amesema Oscar Oscar mchambuzi mahiri wa soka nchini

cut

Mara kwa mara Amunike amekuwa akilaumiwa kwa kutopanga kikosi cha Stars kwa kufuata ubora wa wachezaji waliopo

Amunike pia amekosolewa kwa kuwabadilishia majukumu baadhi ya wachezaji hali inayopelekea wachezaji hao kushindwa kuonyesha ubora wao

Kwenye mchezo wa jana Amunike alimuanzisha John Bocco namba 11 ambapo muda mwingi alikuwa akifanya majukumu ya ulinzi kutokana na Stars kushambuliwa sana

Himid Mao alipangwa namba saba na baadae akamrudisha nafasi ya kiungo baada ya kumtoa Fei Toto

Farid Mussa na Thomas Ulimwengu ambao walianzia benchi, walipoingia waliongeza uhai kwenye safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na Mbwana Samatta na Saimon Msuva ambaye hata hivyo jana alicheza chini ya kiwango kabla ya kufanyiwa mabadiliko

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’