Baada ya mapumziko ya wikiendi, uongozi wa Simba leo utaendelea na zoezi la kuwatambulisha nyota waliosaini mikataba ya kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara
Kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram, Simba imethiitisha kuwa leo saa saba mchana, kifaa kingine kitatambulishwa Msimbazi
Aidha Simba itakamilisha usajili wake wiki hii kwani Juni 30 ndio tarehe ya mwisho ya usajili wa michuano ya CAF
Mchezaji atakayesajiliwa baada ya tarehe hiyo hatakuwa na nafasi ya kucheza michuano ya ligi ya mabingwa mpaka dirisha litakapofunguliwa tena kuelekea hatua ya makundi
ADVERTISE HERE