Simba ilikuwa ikimuwania mshambuliaji wa Al Hilal Idrisa Ilunga Mbombo aliyewahi kuitumikia Zesco United kabla ya kuuzwa msimu uliopita
Hata hivyo inaelezwa usajili wa nyota huyo raia wa DR Congo umekwama kutokana na gharama za kuvunja mkataba wake kuwa kubwa
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Salim Abdallah 'Try Again' amesema gharama za mkataba wa mchezaji huyo ni kubwa kwani ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi ligi kuu ya Sudan
"Gharama ya mkataba wa Mbombo ni kubwa na si yeye tu, bali wachezaji wengi ambao, wanacheza Sudan wanalipwa pesa nyingi ambazo zinachangia ugumu wa usajili wao," amesema Try Again
Simba tayari imekamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Brazil Wilker Da Silva aliyesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara
Mabingwa hao wa ligi kuu mara 20 wanatarajiwa kukamilisha michakato yote ya usajili wiki ijayo