Emmanuel Gabriel ataka umakini usajili Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Jun 2019
Emmanuel Gabriel ataka umakini usajili Simba

Simba imesajili wachezaji wawili wa kigeni, Mbrazil Wilker Henrique da Silva ambaye ni mshambuliaji na kiungo Msudan Sharaf Eldin Shiboub.

Usajili huo ni mpya lakini umemshangaza mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel 'Batgol' ambaye amesema uongozi wa Simba unafanya usajili wake bila kufuata matakwa ya kocha Patrick Aussems.

Batgol ameonyesha kusikitishwa na madai ya kuachwa kwa kiungo Mghana, James Kotei na kusajili nyota hao ambao alidai amewafuatilia viwango vyao ni vya kawaida sana na hawastahili kucheza klabu kama Simba ambayo ina malengo makubwa.

"Unamuacha mchezaji mzuri kama Juuko, Kotei, Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi, Deogratius Munishi 'Dida' unakwenda kusajili Wasudan na Wabrazil, wanatupeleka wapi, inashangaza na kufikirisha kidogo.

"Hata kama hawana nidhamu pengine kama ninavyosikia lakini je kazi yao si wanafanya ama hawafanyi, sidhani kama kuna haja ya kuangalia hilo wakati kazi zao wanafanya vizuri, huu usajili hasa wa wachezaji wa kigeni sikubaliani nao kabisa, ni wa mihemko na matakwa yao," anasema Bagtol

Mchezaji huyo alikwenda mbali kwa kusema;

"Ukiangalia usajili wa Simba na Yanga, Yanga wanasajili vizuri kwa kufuata maelekezo ya kocha wao Mwinyi Zahera hata wakija kuchemka mzigo utamwangukia kocha wao na sio Simba.

"Wamesajili Beno Kakolanya ambaye ameachwa Yanga kwa utovu wa nidhamu, huyo ana tofauti gani na hao akina Niyonzima, Okwi na wengineo kwenye suala la nidhamu?

"Nadhani ifike mahala Mohamed Dewji atumie vizuri pesa zake, zisiwasumbue kwa kukusanya tu wachezaji na kuanza upya kuitengeneza timu, hii itawasumbua na hawatafika mbali michuano ya ndani na nje"

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’