Uongozi wa Simba unasubiri muda muafaka kumtambulisha kiungo Ibrahim Ajib aliyerejea nyumbani
Mkataba wa Ajib na Yanga unamalizika Juni 30, bila shaka Julai mosi kila kitu kitawekwa hadharani
Ajib aliyekuwa nahodha wa Yanga, aligoma kusaini mkataba kuendelea kuichezea timu hiyo licha ya viongozi wa Yanga kufanya juhudi za kumshawishi kupitia mama yake
Ajib alisaini mkataba wa awali na Simba hata kabla ya kupata ofa kunako klabu ya TP Mazembe
ADVERTISE HERE