Inaelezwa klabu ya TP Mazembe imevutiwa na beki wa kushoto wa Simba Mohammed Hussein 'Tshabalala' na imeanza mchakato wa kutaka kumsajili
Msimu uliopita Tshabalala alin'gara na kikosi cha Simba kilichofika hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Kwa sasa yuko Misri na timu ya Taifa inayoshiriki fainali za Afcon 2019 ikitarajiwa kushuka dimbani kesho Jumapili kuumana na Senegal
Nahodha huyo msaidizi wa Simba ni miongoni mwa nyota waliomaliza mikataba na mchakato wa kumpa mkataba mpya unaendelea
Maafisa wa TP Mazembe wako nchini kukamilisha usajili wa nyota wa Mbeya City Eliudi Ambokile
ADVERTISE HERE