Aussems afunguka ujio wa Da Silva

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jun 2019
Aussems afunguka ujio wa Da Silva

Kocha MKuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema kwamba ndoto yake ya kuwa na nyota wa nje ya Bara la Afrika ndani ya kikosi chake, imetimia baada ya kutua kwa ‘kifaa’ kutoka Brazil, Wilker Henrique da Silva ambaye jana alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Aussems amesema kuwa mchezaji huyo ni miongoni mwa nyota ambao aliwataka ndani ya kikosi chake na hivyo kuwaomba mabosi wa Simba kufanya kila wanaloweza kumsajili.

"Simba ni timu ambayo ipo kwenye kiwango cha juu kwa sasa katika klabu za Afrika Mashariki, nilitaka mchezaji wa nje ya Bara la Afrika ili kuboresha kikosi changu, ninaamini sasa itakuwa tishio zaidi," Aussems amenukuliwa na gazeti la Bingwa

Alisema mshambuliaji huyo ni moto wa kuotea mbali ambapo alikuwa akimfuatilia katika mechi za huko Brazil na kwamba alikuwa akifanya vizuri, hivyo anaamini kuwa hatamwangusha.

Mbelgiji huyo alisema inawezekana mashabiki wa Simba, walikuwa na hofu juu ya mbadala wa aliyekuwa mshambuliaji mkongwe wa timu hiyo, Emmanuel Okwi, akiwahakikishia Da Silva ni zaidi ya Mganda huyo. 

Pamoja na kupata mafanikio makubwa msimu uliopita kwa kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imeonekana kujipanga vilivyo kuhakikisha msimu ujao wanakuwa moto zaidi.

Ili kutimiza malengo yao hayo, klabu hiyo imeshamalizana na wachezaji wake wote wa zamani waliopo katika mpango wa Aussems, huku ikiwa imeanza kusajili wapya, wazawa na wa kigeni.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’