Kikosi cha Simba hadharani wiki ijayo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jun 2019
Kikosi cha Simba hadharani wiki ijayo

Klabu ya Simba inatarajiwa kukamilisha usajili wake wiki ijayo ambapo kikosi cha timu hiyo kitawekwa hadharani baada ya zoezi hilo kukamilika

Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema kwa sasa yanayozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu baadhi ya wachezaji kuachwa yatabaki kuwa tetesi

"Mashabiki wetu wawe na subira, usajili ukikamilika kila kitu kitawekwa hadharani," amesema

"Tutaendelea kutambulisha wachezaji wetu kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii na pengine wiki ijayo kazi hiyo ya usajili itakamilika"

Juni 30 ndio tarehe ya mwisho ambayo Simba, Yanga, Azam Fc na KMC zimetakiwa kuwasilisha usajili wao kwani dirisha la usajili la CAF litafungwa Julai mosi 2019

Simba imewaongezea mikataba Aishi Manula, John Bocco, Erasto Nyoni, Jonas Mkude na Meddie Kagere huku ikiwasajili wachezaji wapya Beno Kakolanya, Ibrahim Ajib, Kennedy Juma, Miraji Athumani, Sharifa Eldin Shiboub na Wilker Henrique da Silva

Zoezi hilo la usajili inaelezwa limekamilika kwa asilimia kubwa ambapo nyota wengine wa kigeni na wa ndani waliosaini mikataba watatambulishwa wiki ijayo

Gumzo kwenye mitandao ya kijamii ni taarifa za kutoongezewa mikataba kwa viungo James Kotei na Haruna Niyonzima ambao inaelezwa kuwa ni miongoni mwa nyota ambao wataachwa

Wengi wametoa maoni kubwa Simba itafanya makosa makubwa kama itawaacha wachezaj hao waliokuwa na mchango mkubwa msimu uliopita

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’