Taarifa za uhakika ni kuwa Simba imemsajili winga Miraji Athumani kutoka Lipuli Fc, nyota huyo ameingia kwenye foleni ya kusubiri utambulisho rasmi kama ilivyo kwa nyota wengine waliosaini
Hata hivyo Miraji sio mgeni kwa klabu ya Simba, alilelewa kwenye kikosi cha timu ya vijana na nyota wengine kama Ibrahim Ajib, Abdi Banda, Said Ndemla na nyota wengine kibao
Hivyo kurejea kwake Simba ni kama amerudi nyumbani
Winga huyo aliyen'gara kwenye kikosi cha Lipuli msimu uliomalizika kwenye ligi na michuano ya kombe la FA, amesema ujio wake haukutokea kwa bahati mbaya
Anaamini uwezo alioonyesha na klabu ya Lipuli umemshawishi kocha Patrick Aussems kumsajili
Atahakikisha hamuangushi kocha huyo raia wa Ubelgiji
"Sina wasiwasi najua nitapata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Simba," amesema
"Najua haitakuwa rahisi kwa sababu Simba ina nyota wengi wenye uzoefu na uwezo mkubwa lakini hata mimi naamini kocha ameona kitu kwangu ndio maana akanisajiri"
"Muhimu nikipewa nafasi nitahakikisha nafanya kile ambacho benchi la ufundi litanielekeza"
Miraji anatua Simba kuchukua nafasi ya Shiza Kichuya ambaye aliuzwa nchini Misri