Baada ya mapumziko ya wikiendi, uongozi wa klabu ya Simba leo Jumatatu unaendelea kutambulisha wachezaji waliosaini mikataba kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara msimu ujao
Utaratibu huo uliojizolea umaarufu tangu kuanzishwa kwake, unafanyika saa saba kamili mchana
Msimu huu wa usajili Simba imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuficha michakato yake ya usajili, na kuwafanya wadau wake kusubiri taarifa kutoka kwa uongozi
Kwani taarifa nyingi zinazoripotiwa na vyombo vya habari zaidi ni tetesi
Mpaka sasa John Bocco, Aishi Manula, Jonas Mkude, Erasto Nyoni na Beno Kakolanya tayari wametambulishwa kusaini mikataba ya kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara
ADVERTISE HERE