Mzee Kilomoni ataja sababu ya kuhudhuria hafla ya Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Jun 2019
Mzee Kilomoni ataja sababu ya kuhudhuria hafla ya Yanga

Jana anayejiita mdhamini wa klabu ya Simba Mzee Hamisi Kilomoni alihudhuria tukio la kuchangishana la Yanga lililofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam

Kilomoni ambaye hivi karibuni ameingia kwenye mgogoro na Simba akidaiwa kukwamisha mchakato wa mabadiliko kutokana na kuzuia baadhi ya nyaraka ambazo zinahitajika na mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji 'Mo', amesema alihudhuria hafla hiyo ikiwa sehemu ya kudumisha ushirikiano baina ya Simba na Yanga

Amesema kuonekana kwake ukumbini na watu wa Yanga haimaanishi kuwa amehamia huko

" Mimi ni mdhamini wa Simba na muasisi wa mambo mbalimbali katika klabu hii, Kufika hapa haimaanishi nimehamia Yanga," alisema

"Ngoja niwaambie zamani Yanga na Simba tulishirikiana katika kila jambo upinzani wetu ni uwanjani sio kama sasa vijana wa leo mnaleta uadui

"Ilikuwa kama akifariki shabiki wa Yanga basi mashabiki wa Simba ndio watakaomzika hivyo hivyo akifariki shabiki wa Simba pia Yanga watamzika, haiwezi kuwa busara ndugu zangu wakawa na shughuli hapa hapa Dar nami nisiweze kufika"

Baada ya kuonekana ukumbini na watu wa Yanga jana, wengi wamemtuhumu kuwa huenda akawa anatumiwa na baadhi ya watu kuivuruga Simba

Mzee Kilomoni ambaye alinusurika kufutiwa uanachama kwenye Mkutano Mkuu uliopita, kwa mgogoro anaojaribu kuutengeneza, huenda akafutiwa uanachama wake

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’