Baada ya Kikwete kuipa Simba uwanja, Makonda nae awapa Yanga uwanja

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Jun 2019
Baada ya Kikwete kuipa Simba uwanja, Makonda nae awapa Yanga uwanja

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ameahidi kuipa klabu ya Yanga eneo la kujenga uwanja Kigamboni jijini Dar es salaam

Makonda ameyasema hayo leo katika Harambee ya kuichangia Yanga iliyofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam

Mapema katika hafla hiyo, Rais Mstaafu awamu ya Nne Dk Jakaya Kikwete alisema kuwa alitoa fedha Milioni 30 zilizonunulia eneo la uwanja wa Simba ulioko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam

Dk Kikwete alisema wakati huo Simba ikiwa chini ya Mwenyekiti Ismail Aden Rage, viongozi walimfuata ofisini kwake wakamuomba awachangie kiasi hicho cha fedha waweze kununua eneo hilo la uwanja

Makonda amesema Wanasimba wanatambua mchango wa Dk Kikwete na wanauthamini na kuonyesha kwamba jambo alilolifanya lilikuwa na thamani kubwa, nae ameahidi kuwapa Yanga eneo la kujenga uwanja Kigamboni

Amewataka viongozi wa Yanga wafike ofisini kwake siku ya Jumatatu wakiwa na nyaraka za klabu ili waende wakakabidhiwe eneo hilo

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’