Simba imekuja na utaratibu wa kipekee wa kuwatambulisha wachezaji wake wapya saa saba mchana kila siku
Mpaka sasa nyota watano Aishi Manula, Beno Kakolanya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni na John Bocco tayari wametambulishwa kumwaga wino Msimbazi huku orodha ya nyota wengine ikiendelea kutolewa kila siku
Baadhi ya nyota hao ni pamoja na Ibrahim Ajib aliyekuwa nahodha wa Yanga ambaye inaelezwa tayari amemalizana na Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili
Mwingine ni mshambuliaji wa Nkana Fc Walter Bwalya ambaye naye inaelezwa usajili wake tayari umakamilika

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinasema Simba huenda ikasajili nyota wasiopungua wanne wa kigeni. Usajili wa wachezaji wote unatarajiwa kukamilika ndani ya siku 10
Ikumbukwe usajili kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika unatakiwa uwe umekamilika kabla ya Juni 30 2019
Hata hivyo wakati akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori alisema usajili wa nyota wa kigeni utakuwa wa mwisho kutambulishwa
Kwa sasa wanatambulisha usajili wa nyota wa ndani, wapya na wale waliomaliza mikataba
Emmenuel Okwi, Mohammed Hussein na Shomari Kapombe nao inaelezwa tayari wamesaini mikataba mipya, wako kwenye orodha ya nyota wanaosubiri kutambulishwa
Usajili wa Okwi inaelezwa umekamilishwa baada ya uongozi wa Simba kufanikiwa kumshawishi asaini mkataba baada ya hapo awali kugoma akitaka zoezi hilo lifanyike baada ya michuano ya AFCON 2019 kumalizika