Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori leo amefafanua utata uliojitokeza juu ya usajili wa nahodha wa timu hiyo John Bocco ambaye klabu ya Polokwane City ilidai kumsajili
Magori amesema jambo hilo limekwisha kwa kuwa timu ya Polokwane ya Afrika Kusini inayodai kuwa na mkataba na mchezaji huyo, haikufuata utaratibu.
Magori amesema kwa ukubwa wa Simba sasa hivi, Bocco hawezi kwenda Polokwane ili tu akacheze nje ya nchi.
"Walipokubaliana sisi hatukuwepo, mchezaji amewageuka sasa hivi wanakuja kwetu, kwa hiyo Bocco aiache Simba aende Polokwane, kwa kigezo iko South Afrika!! Hawezi kuondoka, Simba ni timu kubwa"
Magori anasema baada ya Polokwane kushindwa kumpata Bocco, wameomba kupewa mchezaji mwingine wa Simba hata kwa kwa mkopo, Simba ipo tayari kwa mazungumzo