Simba kuharakisha mchakato wa mabadiliko

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Jun 2019
Simba kuharakisha mchakato wa mabadiliko

Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema klabu hiyo imeteua wajumbe wanne ambao watasimamia na kukamilisha mchakato wa mabadiliko kwa vipengele vichache vilivyobaki

Akizungumza na waandishi wa habari leo Hotel ya Serena jijini Dar es salaam, Magori amewataja wajumbe hao ni Aziz Kivile, Mulamu Ng'ambi, Babra Gonzalez na Wanasheria wa Simba

Magori amesema wajumbe hao watafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mchakato unakamilika ndani ya mwezi mmoja

Azungumzia usajili

Magori amesema jana Bodi ya Simba ilipokea ripoti ya Kamati ya Usajili ambapo amesema baadhi ya wachezaji wataachwa na wengine watatolewa kwa mkopo

Usajili wa wachezaji ambao walimaliza mikataba tayari umekamilika huku timu hiyo pia ikiwa tayari imewasajili wachezaji wapya wa ndani

Kuhusu wachezaji wa Kimataifa, Magori amesema zoezi hilo litafanyika katika siku kumi zijazo

Magori amesema wachezaji wa Kimataifa watakaosajiliwa watakuwa bora zaidi ya wale ambao wataachwa na timu hiyo

Aidha amesema orodha ya wachezaji ambao wataachwa au kutolewa kwa mkopo itatolewa baada ya kufanya nao majadiliano

Amesema wataendelea na utaratibu wa kutambulisha mchezaji mmoja mmoja aliyesaini mkataba wa kuitumikia Simba kupitia kurasa maalum za Simba kwenye mitandao ya kijamii

Amkaanga Mzee Kilomoni

Magori amesema Mzee Kilomoni sio Mdhamini wa klabu ya Simba.

Aidha amesema baada ya yeye kukataa kutoa hati ya majengo, Simba ilifanya utaratibu wa kupata hati nyingine

Hivyo hati hiyo inayoshikiliwa na Mzee Kilomoni haiwezi kuzuia mabadiliko yanayofanywa na klabu hiyo

"Hiyo hati iliyoshikiliwa haiwezi kuzuia mabadiliko ndani ya Simba… Hawa wazee siyo walioianzisha Simba, walioianzisha walishakufa, na wao watakufa, na hata sisi tutakufa, watakuja wengine"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’