Mlinda lango Deogratius Munishi 'Dida' huenda asiongezewe mkataba kunako klabu ya Simba baada ya timu hiyo kukamilisha usajili wa Beno Kakolanya aliyekuwa mchezaji huru
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinadai Kakolanya tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara
Dida hakuwa na msimu mzuri ndani ya kikosi cha Simba kwani alishindwa kupata nafasi ya kutosha mbele ya Aishi Manula ambaye tayari ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Simba
"Kuna mazungumzo yanaendelea na moja ya timu kutoka nje ya nchi, kama hayakufanikiwa basi nitajiunga na timu yoyote hapahapa nchini ambaye tutafikia nayo makubaliano," amesema
Dida alijiunga Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja akitoka klabu ya Turks fc inayoshiriki ligi daraja la kwanza huko Afrika Kusini