Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameutaka uongozi wa timu hiyo kumuongezea mkataba kiungo mkata umeme James Kotei
Baada ya kuenea taarifa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Kotei ni miongoni mwa wachezaji waliopendekezwa kuacha na Aussems, Mbelgji huyo amezikana taarifa hizo
"Nimeshangazwa na taarifa zinazoenea mitandaoni eti nimesema katika ripoti yangu mchezaji James Kotei aachwe namheshimu sana Kotei ni kiungo bora hivi naweza pendekeza mchezaji kama huyo aachwe?" amehoji Aussems
Kotei amemaliza mkataba kunako klabu ya Simba na amekuwa akihusishwa kuwaniwa na Kaizer Chiefs inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini
ADVERTISE HERE