Klabu ya Polokwane City inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini imedai ilishakamilisha usajili wa nahodha wa Simba John Bocco aliyesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo mapema leo imebainisha kuwa Bocco ni mchezaji wao ambaye walimsajili kihalali baada ya kumaliza mkataba na Simba
Jana Simba ilitangaza kumuongezea Bocco mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara
Bado uongozi wa Simba haujatoa taarifa rasmi kujibu madai hayo ya klabu ya Polokwane City ambayo imetoa picha na uthibitisho wa mkataba ambao Bocco amesaini

ADVERTISE HERE