Licha ya taarifa kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii hapo jana kuwa kiungo Ibrahim Ajib ameongeza mkataba klabu ya Yanga, inaelezwa kinara huyo wa pasi za mabao msimu uliomalizika amekamilisha usajili wake na Simba
Taarifa za uhakika zimebainisha kuwa Ajib alifanya mazungumzo na Simba na akasaini mkataba wa awali kabla ya ligi kumalizika
Kilichokuwa kinasubiriwa ni kuanza kwa mchakato wa usajili katika klabu ya Simba ili asaini
Inaelezwa kuwa Ajib tayari alikuwa amechukua sahemu ya fedha za usajili alizokuwa ametengewa
Ajib aliachana na mpango wa kujiunga na TP Mazembe baada ya timu hiyo kushinwda kuifikia ofa aliyokuwa amepewa na Simba
Ni suala la muda tu kabla ya kiungo huyo kutangazwa rasmi kuwa mali ya Simba
ADVERTISE HERE