Msimu wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliomaliza ulikuwa mzuri sana kwa washambuliaji watatu wa Simba Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi
Ulikuwa ni msimu wa mabao kwa wakali hao wa kuzifumania nyavu
Watatu hao waliweka rekodi ya kuzifumania nyavu, peke yao wakiweka kambani mabao 54
Mabao 23 ya Kagere, 16 ya Bocco na mabao 15 ya Emmanuel Okwi
Hii ni rekodi ambayo haikuwahi kuwekwa na safu yoyote ya ushambuliaji kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara
Hivihivi ilivyo safu ya ushambuliaji ya Simba, inaweza kuubakisha tena ubingwa msimu ujao kwa msimu wa tatu mfululizo
Wakati Kagere akiwa bado ana mkataba na Simba, Bocco na Okwi wamemaliza mikataba yao
Kwa upande wa Bocco inaelezwa tayari ameongeza mkataba wa mwaka mmoja wakati mazungumzo ya kumbakisha Okwi yanaendelea vizuri
Okwi ametaka kusaini mkataba mpya baada ya kumalizika kwa michuano ya AFCON inayofanyika nchini Misri
Okwi na Juuko Murshid wako kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda