Mshambuliaji aliyeaminiwa sana kwenye kikosi cha Simba Laudirt Mavugo leo amekuwa shujaa wa timu hiyo baada ya kuifungia bao la ushindi katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye dimba la Kambarage Jumapili jioni.
Katika mchezo huo Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 hivyo kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya michezo yote ya mzunguuko wa tano kukamilika.
Simba ikicheza kandanda safi la pasi fupifupi ilianza kuandika bao la kuongoza kwenye dakika ya 16 likiwekwa kambani na Shiza Kichuya.
Bao la pekee la Stand United lilifungwa na Mtasa kwenye dakika ya 51 baada ya kumalizia mkwaju wake wa penati uliokuwa umepanguliwa na Aishi Manula.
Stand United ilipata penati hiyo baada ya Ally Shomari kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe alama 11 sawa na Mtibwa na Azam FC lakini imekwenda kileleni kutokana na uwiano mzuri wa mabao (+11)
Ligi kuu ya Vodacom itaendelea baada ya wiki mbili kupisha michuano iliyo kwenye kalenda ya FIFA.

ADVERTISE HERE