Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Emmanuel Amunike amewaondoa Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu katika kikosi cha wachezaji 32 wanaosafiri kwenda Misri tayari kwa michuano ya AFCON 2019
Amunike amesema kigezo kilichotumika kuwaacha nyota hao ni kiwango chao mazoezini na nidhamu
Amunike amesisitiza anajua watu wanamatamanio yao juu ya wachezaji fulani lakini nidhamu na utimamu wa viwango vyao katika mazoezi ni kipaumbele kikubwa ukiachana na Kapombe ambaye bado hajarudi kwenye ubora wake
Pia kocha huyo amewajumuisha makinda Kelvin John na Boniphace ili kuwapa uzoefu zaidi.
Wachezaji wengine walioachwa ni pamoja na Ayoub Lyanga, Ally Khamis, Kennedy Wilson, Ally Ally na Shomari Kapombe
ADVERTISE HERE