Aussems kukatisha likizo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Jun 2019
Aussems kukatisha likizo

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems anatarajiwa kurejea mapema kuanza maandalizi ya kikosi chake kuelekea michuano ya msimu ujao

Msimu ujao Simba itashiriki Ligi Kuu, Kombe la FA na michuano ya Ligi ya Mabingwa

Kwa mujibu wa kalenda iliyotolewa na CAF, michezo ya hatua ya awali ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho itafanyika mwanzoni mwa mwezi wa nane

Simba wakiwa mabingwa wa Tanzania Bara, pia watashiriki michuano ya kombe la Kagame inayoanza Julai 7 mpaka Julai 21 2019

Aussems aliondoka wiki iliyopita kuelekea kwao Ubelgiji kwa ajili ya mapumziko baada ya kumaliza msimu kwa mafanikio makubwa, akiiongoza Simba kutwaa ubingwa pamoja na kufika robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

cut

Katika hatua nyingine, Aussems amesema ongezeko la timu za Tanzania kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika pamoja na kombe la Shirikisho, litaongeza ushindani kwenye ligi hivyo ametaka kufanyika maandalizi kabambe kabla ya msimu kuanza

"Tanzania kupeleka timu mbili katika hii michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ni faraja kubwa na ndio ukomavu wa soka, lakini tayari hapo kuna ushindani mkubwa ambao inabidi nipambane kuhakikisha wasifu wa Simba unabaki juu zaidi," amesema Aussems

"Mpaka nimepewa mkataba mpya, Simba wameniamini na wameridhika na kazi ambayo niliifanya msimu uliopita, hivyo lazima nipambane zaidi kuhakikisha ninatimiza kile ambacho wanakihitaji"

"Msimu ujao tutakuwa tukicheza na presha, maana Yanga wakianza kushinda, na sisi tutakuwa na presha ya kushinda pia, hii ni hatari, tunatakiwa kujipanga hasa"

Mafanikio iliyopata Simba kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliomalizika, yameiwezesha Tanzania kuongezwa idadi ya timu zinazoshiriki michuano ya CAF kutoka mbili na kuwa nne

Yanga na KMC zimenufaika na mafanikio hayo ambapo Yanga sasa inaungana na mabingwa wa ligi kuu Simba kushiriki ligi ya mabingwa na KMC inaungana na mabingwa wa kombe la FA Azam Fc kushiriki kombe la Shirikisho

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’