Beki wa Simba Shomari Kapombe hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa inayoelekea nchini Misri kushiriki michuano ya AFCON 2019 inayoanza Juni 21 mpaka Julai 09 2019
Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema beki huyo ameenguliwa kutokana na majeraha yanayomkabili ili ajiimarishe zaidi kiafya
Dalili za Kapombe kuondolewa timu ya Taifa zilianza juzi baada ya TFF kutoa taarifa kuwa mchezaji huyo alijitonesha jeraha kwenye mazoezi ya timu ya Taifa
Hata hivyo Kapombe alikanusha taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji wa TFF Clifford Ndimbo na kutoa ufafanuzi wa sintofahamu iliyokuwa imejitokeza
Kwa sasa Kapombe anaendelea na program ya mazoezi aliyoachiwa na benchi la Ufundi la Simba na baada ya kuenguliwa Stars, atakuwa na muda zaidi wa kujiimarisha na kuwa fiti kuelekea msimu ujao