Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limeagiza kurudiwa kwa mchezo wa pili wa fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Esperance dhidi ya Wydad Casablanca uliovunjika wiki iliyopita nchini Tunisia
Esperance ilikuwa tayari imekabidhiwa taji la ubingwa baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 (agg 2-1) katika mchezo uliovunjika dakika ya 59 baada ya Wydad kukataliwa bao halali huku VAR ikiwa haifanyi kazi
"Mazingira ya mchezo na ulinzi hayakuwa ya kuridhisha hali iliyopelekea mchezo kuvunjika," alisema mshauri wa Rais wa CAF baada ya kikao cha mabosi wa CAF kilichofanyika jijini Paris
"Sasa mchezo utarudiwa kwenye uwanja huru nje ya Tunisia. Esperance wanapaswa kurudisha kombe na medali"
"Mchezo utapigwa baada ya michuano ya AFCON kumalizika"
Klabu ya Esperance inatarajiwa kuukatia rufaa uamuzi huo