Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba Sc Bilionea Mohammed Dewji 'Mo', licha ya kukabiliwa na majukumu mengi, amekuwa karibu sana na jamii
Mo amejipambanua kwa kuthamini mpaka vile vitu vidogo vidogo ambavyo vinaweza kuonekana havina maana
Leo amefichua kuwa amekuwa akipokea michoro ya picha zake alizochorwa na wasanii mbalimbali
Na hutunza michoro hiyo kuthamini kazi vipaji na muda wanaotumia wachoraji hao
"Nawashukuru sana wote wanaotumia muda wao kunichora. Nashangazwa na namna walivyo na vipaji vikubwa. Nimeziweka picha zote ukutani kutambua kazi zao kwa sababu natambua ugumu wa utaalamu huu na juhudi walizofanya ili kunichora," ameandika Mo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

ADVERTISE HERE