Kapombe aishangaa TFF

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Jun 2019
Kapombe aishangaa TFF

Beki wa Simba Shomari Kapombe ameshangazwa na taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) juu ya majeraha yake

Taarifa iliyotolewa mapema leo na TFF ilidai kuwa Kapombe alitonesha majeraha wakati akiwa mazoezi na kikosi cha timu ya Taifa hivyo anaweza kuondolewa kwenye timu hiyo inayojiandaa na fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika Misri Juni 21

Hata hivyo Kapombe amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na anaendelea na program ya mazoezi aliyoachiwa na kocha wa Simba

"Taarifa ya mimi kutonesha majeraha imenisikitisha sana kwa kuwa haina ukweli wowote," amesema Kapombe

"Mimi nilipewa program maalum na kocha wangu wa Simba, sasa kwa kuwa michuano hii ya AFCON ninayotakiwa kwenda kushiriki inahitaji niwe fiti, nilipeleka mapendekezo kwa benchi la ufundi la Stars nikiomba niendelee na program ya mwezi mzima ambayo nimeachiwa na kocha"

"Lakini hawakunijibu na badala yake wametoa taarifa hii"

"Niwahakikishie wadau wa soka na mashabiki wa Simba kuwa mimi niko fiti, naendelea na program niliyoachiwa na kocha wa Simba"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
5h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
11h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
14h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’